Usiende Less | Ep 02

0
Tuliishia Combo akila kichapo na hatujui mpigaji ni nani na kwanini mkali vile
Sasa tuendelee na mkasa wetu wa kuvutia ikiwa ni Episode ya pili

Mussa na Lava walifika wakajiona tukio lote lakini walibaki wakimcheka tu😂

Usichokijua ni kwamba Lava ni marioo ambaye analelewa na yule mke tuliyemuona Episode ya kwanza
Sasa leo huyu mwanamke alikutana na mdogo wake wa kike na yule binti alikuwa akichukizwa na mambo ya dada yake kuishi na kijana Lava
Alimshauri mengi ikiwemo umri wa mwanamke kuwa mkubwa kwa Lava

Upande mwingine tutawaona Lava na Combo wakishauliana kuhusu maisha ya ndoa na Combo akitoa ushauri ambao Lava hakuupenda

Mussa anampa Combo mzigo apeleke sehemu na kule anapewa kiasi kidogo apelekee familia yake

Mambo mengi sana utayaona hivyo twende sawa ili kufaidi uhondo wa filamu hii ya 'Usiende Less'

Lava ndoa yake imeishaingia doa na alijichanganya akampiga mwanamke wake jambo ambalo lilimgharimu
Alifukuzwa na hata rafiki zake walipokuja kumtetea waliishia kutukanwa tu

Combo analeta mademu ofisini kwa Lava kisha anawatoroka na kumuachia Lava na pesa hajawalipa

Fuatilia mkasa huu mpaka mwisho ili kuelewa nini kipo ndani zaidi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)