Kunihusu Mimi

Habari, mimi ni Zephiline F Ezekiel, mtaalamu wa masuala ya mitandao ya kijamii. Kupitia tovuti hii, nataka kuwajulisha watembeleaji wangu kuwa ninaweza kuwasaidia kufungua na kutatua changamoto za YouTube Channel, Twitter Account, Facebook Page, Tik Tok Account, Instagram Account n.k

Mitandao ya kijamii ni njia nzuri ya kujitangaza, kujifunza, kujenga uhusiano na kufanya biashara. Lakini pia ina changamoto zake, kama vile kudhibitiwa(hack), kufungiwa, kupoteza nywila(password) au kupata maoni hasi. Kama unakabiliwa na changamoto yoyote kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii, usihofu. Mimi niko hapa kukusaidia kutatua matatizo yote yanayoweza kutokea kwenye akaunti hizo.

Pia wale wa youtube ninaweza kusaidia mtu hatua zote mpaka anaanza kulipwa. Kukuza akaunti kwa kumsambaza na kutengeneza matangazo ya video ili upate watembeleaji wengi. Youtube ni jukwaa la video ambalo linaweza kukuletea mapato mazuri ikiwa utazingatia vigezo na masharti yake. Mimi nina uzoefu wa miaka mingi katika kuendesha na kukuza youtube channel. Nitakufundisha jinsi ya kupata watazamaji, kuongeza ubora wa video zako, kuweka maneno muhimu na kujiunga na mpango wa matangazo.

Ikiwa unakabiliwa na changamoto yoyote kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii, au ikiwa unataka kukuza chaneli yako ya YouTube, tafadhali wasiliana nami:
Unaweza pia kunifollow kwenye mitandao yangu ya kijamii ambayo nimeorodhesha hapo chini. Nitafurahi sana kukusikia na kukusaidia. Asante kwa kutembelea blogu yangu.

X(Twitter)
Facebook

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)